Home Sports MECHI SITA ZA UGENINI ZA YANGA,NNE KUPIGWA NJE YA DAR

MECHI SITA ZA UGENINI ZA YANGA,NNE KUPIGWA NJE YA DAR

BAADA ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wakiwa ni vinara na pointi zao 39 sasa wamebakiwa na mechi 6 ugenini na nne wanatarajiwa kuzicheza nje ya Dar.

Katika mechi 15 mzunguko wa kwanza Yanga ilicheza mechi 9 ugenini na nyumbani ilicheza mechi 6, ilishinda mechi 12, sare 3 huku ikitupia jumla ya mabao 25.

Mzunguko wa pili Yanga itacheza mechi 6 ugenini na 9 ikiwa nyumbani na ni mechi nne tu itawalazimu Yanga kusepa Dar es Salaam.

Mechi hizo ni dhidi ya Geita Gold,Biashara United ya Mara, Mbeya City ya Mbeya na Dodoma Jiji.

Mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa Dar ni dhidi ya Ruvu Shooting na Azam FC.Upo uwezekano wa mechi hizo kuweza kuchezwa nje ya Dar ikiwa timu zitaomba kuweza kuchezwa nje ya Dar.

Ni Kocha Mkuu, Nasreddien Nabi ambaye anakiongoza kikosi hicho chenye maskani yake Jangwani.

Nabi ameweka wazi kwamba anahitaji pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza ndani ya ligi.

Previous articleSIMBA YATOA UJUMBE HUU KUHUSU LIGI KUU BARA
Next articleBARCELONA WAINYOOSHA NAPOLI