AIR MANULA NI NAMBA MOJA

AISHI Manula, ‘Air Manula’ kipa wa Simba ni namba moja kwa makipa waliokaa langoni kwenye mechi zote 15 za mzunguko wa kwanza na kusepa na clean sheet, (cheza bila kufungwa) nyingi.

Manula amekaa langoni kwenye mechi zote 15 ambazo Simba imecheza na amefungwa mabao 6 katika mechi hizo ambazo amekaa langoni.

Katika mechi hizo ni mechi 9 pekee hakuweza kutunguliwa alipokuwa akitimiza majukumu yake kwenye mechi za ligi.

Aboutwalib Mshery wa Yanga anafuata ambapo  alianza maisha yake ndani ya Mtibwa Sugar na sasa yupo Yanga ambapo ni kipa namba mbili.

Ana jumla ya clean sheet 8 na Diarra Djigui wa Yanga yeye ni namba tatu ana clean sheet 7.

Musa Mbisa wa Coastal Union ya Tanga inayotumia Uwanja wa Mkwakwani Tanga yeye ni namba nne akiwa amekusanya clean sheet 6 kibindoni.

Ahmed Salula wa Azam FC inayotumia Uwanja wa Manungu Complex yeye ana clean sheet 5 sawa na Metacha Mnata wa Polisi Tanzania na James Ssetuba wa Biashara United ya Mara.