MMOJA wa mashabiki wa Yanga, mwenye asili ya Kimasai anayefahamika kwa jina la Mauya mkazi wa Dakawa, amemzawadia ng’ombe mzima mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele.
Mayele ni mtupiaji namba moja ndani ya Yanga akiwa na mabao 7 na kinara ni Relliats Lusajo ambaye ametupia kibindoni mabao 10.
Ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana mbele ya Mtibwa Sugar umewafanya Yanga kukamilisha mzunguko wakiwa na pointi 39 kibindoni.
Mayele ambaye alitupia bao moja kwenye mchezo huo amesema kuwa ni furaha kupewa zawadi hiyo na anaamini kwamba atazidi kuongeza juhudi kwenye mechi zijazo.
“Ikiwa nimepewa zawadi kwangu ni furaha na nitazidi kuongeza juhudi kwa ajili ya mechi zijazo ili kupata ushindi,”.