YANGA YAIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ikiwa ni namba moja katika msimamo na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 kituo kinachofuata ni Manungu.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hawana hofu na mchezo huo kwa kuwa maandalizi yapo vizuri.

“Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo vizuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Mtibwa Sugar tunachohitaji ni pointi tatu.

“Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu nasi tutapambana kupata pointi tatu kikubwa mashabiki wetu wajitokeze kupata burudani,”.

Maandalizi ya Yanga kwa sasa yanaendelea katika kambi ya Avic Town iliyopo Kigamboni.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Fiston Mayele,Paul Godfrey, Deus Kaseke,Djuma Shaban na Djigui Diarra.