JOHN Bocco, Nahodha wa Simba, amesema hawatawaangusha Watanzania kwenye mashindano ya kimataifa
kwa kuwa wapo vizuri na watapambana bila kuchoka.
Simba ikiwa Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, leo Jumapili inatarajiwa kutupa kete yake ya
pili mbele ya US Gendarmerie, mechi ikichezwa nchini Niger
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu na kila timu inahitaji ushindi nasi tutapambana kushinda.
“Kwa upande wa ushindi hata wachezaji pia tunapenda na furaha yetu kuona inakuwa hivyo, tutapambana kufanya vizuri, hatutawaangusha Watanzania, kikubwa wao watuombee.”
Katika mchezo dhidi ya ASEC Mimosas, Bocco alitoa pasi moja ya bao kwenye ushindi wa 3-1 Uwanja wa Mkapa.