BAADA ya kucheza mechi 16 bila kupoteza ambazo ni dakika 1,440 Klabu ya DTB ilinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Green Warriors FC ambao waliweza kutibua rekodi hiyo katika mchezo wa 17 uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Februari 13 kwenye Championship.
Wakati huu inajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya African Sports unaotarajiwa kuchezwa leo Februari 19,2022 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwenye msimamo DTB ni namba moja ikiwa na pointi 42 ikiwa imeshinda mechi 13, sare 3 na kupoteza mchezo mmoja.
Inakutana na African Sports iliyo nafasi ya 12 na pointi 19 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 17.
Ni DTB yenye mastaa wengi ambao waliwahi kucheza Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na James Kotei, James Msuva, Juma Abdul na inanolewa na Kocha Mkuu, Ramadhani Nswazurimo ambaye aliwahi kuinoa pia Mbeya City na Singida United.