SAUTI:MAYELE ATOA KAULI YA KIBABE,ATAKA KILA KITU

FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga ameweka wazi kwamba anahitaji kusepa na tuzo za ufungaji bora kwenye mashindano yote ambayo anashiriki kwa msimu wa 2021/22.

Kwenye ligi Mayele ametupia mabao sita akiwa ni kinara kwa upande wa Yanga na pia ametoa pasi mbili za mabao kwa upande wa Kombe la Shirikisho ametupia bao moja ilikuwa ni mbele ya Biashara United.