MASHABIKI wa Simba wameweka wazi kwamba ushindi ambao wameupata wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting wanajua kwamba kuna maombolezo na wote wanaombeleza lakini kwenye mpira Simba wakiwa wanataka kitu lazima kikamilike hivyo wanaomba radhi kwa yaliyotokea.
Ushindi wa mabao 7 Uwanja wa Mkapa unaifanya Simba kutinga hatua ya robo fainali inaungana na Yanga,Pamba,Polisi Tanzania,Azam FC ambazo ni miongoni mwa timu ambazo zimetinga hatua ya robo fainali.