VIDEO:MASAU BWIRE ATAJA SABABU ZA RUVU SHOOTING KUFUNGWA 7-0

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa sababu kubwa ya kupoteza kwa kufungwa mabao 7-0 yametokana na mambo makubwa matatu ambayo yalisababisha wapate matokeo hayo.

Bwire amesema kuwa sababu ya kwanza ilikuwa ni majonzi kwa sababu wachezaji walitoka kumpoteza mchezaji muhimu ambaye alikuwa kwenye kikosi hicho.

Pia amesema kuwa wachezaji wa Ruvu Shooting waliwadharau Simba kwenye mchezo huo na sababu ya tatu ipo kwenye maandiko matakatifu kama ambavyo familia ya Yusuph ndugu zake walitaka kumuangamiza.