SAID Ntibanzokiza, ‘Saido’mambo yake yalikuwa magumu mbele ya Biashara United kwa kushindwa kumtungua kipa namba moja wa Biashara United, James Ssetuba jambo lililofanya kila muda awe anajisikitia anapokosa nafasi.
Juzi wakati Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United na mabao ya Yanga yalifungwa na Yannick Bangala pamoja na Fiston Mayele aliyetumia pasi ya Saido.
Kwenye mchezo huo kiungo huyo alipewa majukumu ya kupiga kona na faulo na aliweza kupiga kona 9,faulo 6 na mapigo yake yote hayo huru hayakuweza kuleta matunda jambo ambalo lilifanya ajisikitie uwanjani.
Ushindi wa timu hiyo inawafanya watinge hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na 2021 iliweza kutinga hatua ya fainali na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye fainali iliyochezwa mwisho wa reli Kigoma, Uwanja wa Lake Tanganyika.
Nabi alisema kuwa makosa ambayo wanayafanya watayafanyia kazi ili kuweza kupata wanachostahili ndani ya uwanja.