UWANJA wa Mkapa Simba imeshinda mbele ya Ruvu Shooting kwa kutupia mabao 7-0.
Kipindi cha kwanza Simba walitupia mabao matano ilikuwa kupitia John Bocco na Clatous Chama ambao walitupia mabao mawilimawili na bao moja ilikuwa ni la kujifunga kwa Michael Masinda ilikuwa dakika ya 44.
Kipindi cha pili Ruvu Shooting walifanya mabadiliko kwa kumtoa kipa Makaka nafasi yake ikachukuliwa na Benedict Tinnoco.
Ni mabao mawili yamefungwa na Chama bao moja na kufikisha mabao matatu ikiwa ni hat trick na Jimsone Mwanuke naye ametupia bao moja.