BAO la Pape Sakho dakika ya 12 linawafanya Simba kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa mbele.
Ni mchezo wa kwanza hataua ya makundi ambapo ni msako wa pointi tatu muhimu.
Itabidi wajilaumu wenyewe ndani ya dakika 45 kwa kukosa nafasi tatu za wazi ambazo wametengeneza kwa kushindwa kuzibadili kuwa mabao.
Nafasi moja ilikoswa na Meddie Kagere aliyegongesha mpira nguzo na ile ya Peter Banda ambaye alipaisha akiwa ndani ya 18.
ASEC Mimosas wanacheza mpira wa kutulia na pasi nyingi Uwanja wa Mkapa.