LWANGA KUWAKOSA ASEC MIMOSAS LICHA YA KUPIGA MATIZI

LICHA ya Taddeo Lwanga kiungo mkata umeme wa Simba kuanza mazoezi hana uhakika wa kuanza kesho mbele ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya makundi.

Kwa sasa Simba ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Lwanga pia ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo katika mazoezi ambayo yanafanyika Uwanja wa Mkapa chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco na Seleman Matola ambaye ni msaidizi.

Sababu ya kuukosa mchezo wa kesho ni kutokuwa fiti kwa kuwa amekosa mechi nyingi za ushindani wakati alipokuwa akitibu majeraha yake.