WAHARIRI WASHUHUDIA MAENDELEO YA KITUO CHA KIGAMBONI

LEO Februari 11,2022 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia pamoja na Wahariri wa Habari za Michezo walitembelea mradi wa Kigamboni.

Karia alipata muda wa kufafanua mambo kuhusu Mradi wa Kituo cha Ufundi Kigamboni kwa Wahariri wa Michezo.

Ikumbukwe kwamba kituo hicho kilichopo Kigamboni kinajengwa na TFF.

Pia mbali na Wahariri wa Habari za Michezo kupata muda wa kushuhudia maendeleo hayo kwa vitendo walipata ufafanuzi wa masuala ambayo walikuwa wanahitaji kuyatambua.