KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco Martín amesema kuwa Katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya ASEC Mimosas watawakosa nyota wao watano kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi.
Wachezaji hao ni mshambuliaji Chris Mugalu ambaye amevunjika mkono hivyo hatahusika katika mchezo huo, Kibu Denis ambaye anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi.
Pia yupo kiungo Clatous Chama hatashiriki kabisa michuano hiyo kutokana na kanuni za (CAF), Thadeo Lwanga majeruhi na Bernard Morrison aliyesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.
Simba, Februari 13, 2022 saa 10:00 jioni watashuka Katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kumenyana na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.