NI zaidi ya umafia! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kile ambacho Benchi la Ufundi la Simba limekifanya katika
maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Katika umafia huo, Simba wamemtumia beki wao wa kati raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye amevujisha mbinu zote za wapinzani wao hao jambo lililomfanya Kocha Mkuu, Pablo Franco, kuanza kutabasamu akiona tayari wamepata pa kuanzia.
Simba Jumapili hii, watakuwa na kibarua cha mchezo wa kwanza wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Wawa amewahi kuichezea ASEC Mimosas kwa kipindi cha miaka nane tangu 2003 mpaka 2011 ambapo
alijiunga na Al Merreikh ya Sudan, kabla ya kutua Azam alipocheza 2014 hadi 2016, kisha akarudi Al Merrikh.
Baada ya hapo, 2017 akatua Simba alipo hadi sasa.
Akizungumza na Spoti Xtra kuhusu wapinzani wao hao, Wawa alisema: “Najisikia furaha kupata nafasi ya
kucheza tena dhidi ya ASEC Mimosas baada ya kupita takribani miaka 12, hii ni timu ambayo ilinipa nafasi ya
kujulikana na kucheza Sudan na sasa Tanzania.
“Utakuwa mchezo mzuri kutokana na ukweli kwamba wachezaji wao wengi wanatokea kwenye vituo vya
kukuzia vipaji.
“Utamaduni wao kwa kiasi kikubwa ni wa kucheza mpira wa kiufundi na kumiliki zaidi mchezo, lakini sio
wazuri sana katika mpira wa nguvu, hivyo kama tutaweza kuwakaba na kuwashambulia kwa nguvu basi ni wazi
lazima tutapata matokeo mazuri dhidi yao.”
Naye Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, alisema: “Tunauelekea mchezo mgumu dhidi ya ASEC Mimosas, lakini niwaweke wazi kuwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda.
“Kupitia njia zetu mbalimbali tumefanya tathimini ya ubora na upungufu wao, hivyo tunajua nini cha kufanya.” Katika Kundi D, mbali na ASEC Mimosas, Simba imepangwa na timu za RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gendarmerie