SIMBA YAWAITA YANGA KUWASAPOTI CAF

UONGOZI wa Simba umewakaribisha mashabiki wa timu mbalimbali ikiwemo Yanga kuwaunga mkono katika mchezo wao wa hatua ya makundi ya Kombe la ShirikishoAfrika dhidi yaASEC Mimosas kutoka Ivory Coast, unaotarajiwa kufanyika Februari 13, katika Uwanja wa Mkapa, Dar.


Simba inatarajiwa kucheza mchezo huo
ambao ni wa kwanza wa Kundi D ambapo timu nyingine ambazo zipo katika kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gerndamarie ya nchini Niger.


Akizungumza na Championi Jumatano,
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba,AhmedAlly, alisema: “Nawakaribisha mashabiki wa timu zote kuja kutushangilia, sio tu mashabiki wa Simba japo naamini kuwa
Simba tuna mashabiki wengi sana ambao
wangetosha kuja lakini hata wale wengine pia mnakaribishwa kuja kutushangilia.


“Kwetu michuano ya kimataifa si jambo
geni na tumezoea kushiriki, safari hii tunahitaji kuona tunafika mbali katika michuano hii, hivyo tumejipanga kupambana katika mchezo huo kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu katika
michuano hii mikubwa baraniAfrika.”