MO BADO YUPO SIMBA,ATINGA KAMBINI

RAIS wa Heshima ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa anaamini timu hiyo itafanya vizuri katika Kombe la Shirikisho kutokana na wachezaji kuwa tayari kwa ushindani.

Februari 13,Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Februari 9,Mo aliweza kuwatembelea wachezaji kambini na kuzungumza nao masuala mbalimbali kuhusu kuweza kufanya vizuri katika mechi za kimataifa na ligi.

Mo amesema”Bado nipo Simba na nimekuja kuongea na wachezaji kuwapa hamasa pamoja na viongozi kuelekea katika mechi zetu lazima tujipange ili kufanya vizuri.

“Kwenye Ligi ya Mabingwa tumeteleza lakini tupo kwenye Kombe la Shirikisho hivyo lazima tujipange ili tuweze kufanya vizuri na kwenye ligi pia.

“Ushindi wa Simba sio wa Mo ni wa mashabiki na kila anayeipenda Simba hivyo tuna kazi ya kufanga huku kimataifa na katika ligi,”.