YANGA WAZITAKA POINTI ZA MTIBWA SUGAR

KIUNGO wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, Dickson Ambundo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga wana kazi ya kusaka pointi mbele ya Mtibwa Sugar ambao watakuwa kwao huku wakiwa na kumbukumbu ya kuishuhudia Simba ikitoka suluhu ilipokwenda kucheza huko hivi karibuni.


Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hivi 
sasa, Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 36, huku Mtibwa ikiwa na pointi 12 katika nafasi ya 14. zote zimecheza mechi 14.

Ambundo amesema: “Maandalizi yetu yapo vizuri kuelekea mchezo huo, tumepata muda wa kupumzika wa kutosha, sasa ni muda wa kujipanga kuwamaliza Mtibwa.

“Kwa upande wangu nimejipanga kupambana kwa hali ya juu ili kuweza kuisaidia timu yangu kupata matokeo
mazuri, ukiangalia tulipata matokeo ya 
sare kwa mchezo uliopita na mchezo huu  tunataka matokeo ya ushindi,”.

Ilikuwa ni mbele ya Mbeya City baada ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-0 Mbeya City wanatarajiwa kucheza ndani ya Manungu, Februari 23.