YANGA:HATUKUKURUPUKA KUFANYA USAJILI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba usajili walioufanya ni wa viwango vikubwa jambo linalowapa matumaini yakufanya vizuri kwenye mashindano ambayo watacheza kwa kuwa hawakukurupuka.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Yanga ni pamoja na Chico Ushindi, Dennis Nkane,Salim Aboubakhari na Crispin Ngushi.

Wachezaji hao wameanza kucheza mechi za ushindani isipokuwa kwa sasa Nkane bado yupo nje kwa muda akitibu majeraha ambayo alipata kwenye mechi za Kombe la Mapinduzi.

Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Thabit Kandoro amesema kuwa walifanya usajili makini utakaowapa matokeo mazuri.

“Usajili wa wachezaji ambao tumewafanya ni wa viwango kwa kuwa kila mchezaji ana uwezo mkubwa na hili itatufanya tuwe imara katika ushindani.

“Uwepo wa Chico, (Ushindi), Nkane,(Dennis) hawa wote wanajua mpira na watafanya jambo ambalo tunahitaji ikiwa ni pamoja na kupata matokeo uwanjani, ” amesema Kandoro.

Chanzo:Spoti Xtra