UONGOZI wa Kampuni ya GSM leo Februari 7, 2022,umetangaza rasmi kujiondoa kwenye nafasi ya kuwa Mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC.
Taarifa ambayo imetolewa na Ofisa Biashara Mkuu wa GSM, Allan Chonjo imeeleza kuwa leo Februari 7,2022 GSM imetangaza rasmi kujiondoa kwenye nafasi ya kuwa mdhamini mweza wa ligi.
Sababu ya kufikia maamuzi hayo ni kwa TFF pamoja na Bodi ya Ligi kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya kimkataba kama pande hizo mbili ambavyo zilikubaliana.
Pia wameongeza kuwa GSM waliridhia kuwa wadhamini ili kuweza kukuza sekta ya mpira wa miguu nchini pamoja na michezo kiujumla lakini haikuwa kama ilivyotarajiwa.
Pia Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Ghalib Said Mohamed amejiuzulu nafasi hiyo.