JUKUMU LA PETER BANDA HILI HAPA

SIMBA imeweka wazi kuwa mara baada ya kiungo mshambuliaji wao, Peter Banda kurejea nchini akitokea Cameroon alipokuwa na kibarua cha kuiwakilisha Malawi kwenye mashindano ya Afcon, moja kwa moja atajiunga na programu za maandalizi ya michezo ijayo hususani mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imepangwa kwenye Kundi D pamoja na timu za RS Berkane ya Morocco, USGN ya Niger na ASEC Mimosas

Mchezo wa kwanza wa Simba katika hatua ya makundi utakuwa Jumapili ya Februari 13 dhidi ya ASEC Mimosas, mwaka huu wakianzia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry, amesema: “Ni kweli tunamtarajia kiungo mshambuliaji wetu Banda kujiunga na kikosi baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa.

“Tunatarajia atajiunga na kikosi ambapo atakuwa sehemu ya programu za kujiandaa na michezo yetu miwili inayofuata hususani ule wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.