KILA LA KHERI TANZANITE, MSITUANGUSHE

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens kimewasili salama Adis Ababa nchini Ethiopia.

Na lengo kubwa la kiweza kufika huko ni kwa ajili ya mchezo wa kuwania kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia.

Utakuwa ni mchezo wa marudio dhidi ya timu ya Wanawake ya Ethiopia kesho Ijumaa, Februari 4 2022.

Muda wa zaidi ya siku 10 ulikuwa ni maandalizi chini ya Kocha Mkuu, Bakari Shime na kambi ilikuwa pale Karatu,Arusha.

Ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza haimaanishi kwamba kazi imeisha hapana tunawaamni,msituangushe.

Ushindi wenu ni muhimu na utafungua matumaini ya kuweza kufuzu fainali safari ya kwenda Costa Rica kushiriki michuano ya Kombe la Dunia.