MBWANA SAMATTA, MSUVA,FEI TOTO KAMILI KUWAVAA DR CONGO

IDADI kamili ya nyota wa timu wa taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen imekamilika baada ya leo Novemba 9, Mbwana Samatta kuungana na wachezaji wenzake.

Pia Simon Msuva yeye alikuwa ndani ya kikosi jana Novemba 8 na leo ameungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Stars ipo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo ina mechi mbili za kwenye Kundi J zote zikiwa zipo karibu.

Itaanza na DR Congo, Novemba 11, Uwanja wa Mkapa kisha kazi inayofuata itakuwa dhidi ya Madagascra nchini Madagascar timu zote zikiwa zipo kundi J ambalo kwa sasa linaongozwa na Stars yenye pointi 7 sawa na Benin iliyo nafasi ya pili.

Mchezo dhidi ya Madagascar unatarajiwa kuchezwa Novemba 14, 2021 hivyo baada ya kumaliza mchezo dhidi ya DR Congo Stars itakwea pipa moja kwa moja na kuunganisha nchini Madgascar kwa ajili ya mchezo huo.

Kwa mujibu wa Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania,Nadir Haroub, ‘Canavarro’ amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari na morali kuelekea mchezo huo ni kubwa.

“Morali ni kubwa na kila mchezaji anahiaji kuona tunapata ushindi hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi ka ajili ya kuwapa nguvu wachezaji,”.