MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Novemba Mosi,2021 wameachia orodha ya wachezaji wao ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora.
Ni Mchezaji Bora wa Mashabiki ambaye anasakwa kwa mwezi Oktoba na tuzo hiyo inadhaminiwa na Emirate Aluminium ACP.
Wanaowania tuzo hiyo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao watapigiwa kura ni pamoja na kiungo wa kazi Sadio Kanoute nyota wao Rally Bwalya mzee wa mipira iliyokufa akiwa ametupia bao moja kwa mkwaju wa penalti ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania.
Yupo pia kiungo mzawa Hassan Dilunga mzee wa kulazimisha mambo ndani ya uwanja.