
TFF, TPLB SOGEZENI MACHO YENU CHAMPIONSHIP…
MWENDO wa Ligi Daraja la Kwanza umeongeza mvuto kwa kiasi kikubwa wakati ligi hiyo ikiwa inakwenda ukingoni. Vinara ni DTB wakiwa na pointi 55 na inavyoonekana kama watashinda mechi zao mbili zilizobaki na kujikusanyia pointi sita, watakuwa na asilimia 95 ya kuwa tayari wamepanda hadi Ligi Kuu Bara. Pointi 61 zinaonekana kuwa uhakika…