
YANGA YATUMA UJUMBE HUU SIMBA
ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, ameweka wazi kuwa, kwa msimu mpya wa 2023/24, malengo yao ni kuendelea pale walipoishia msimu wa 2022/23. Msimu wa 2022/23, Yanga ilikomba taji la Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii na Kombe la Azam Sports Federation, huku ikigotea nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Kamwe amesema wanahitaji…