AZAM FC WATEMBEZA MKWARA HUU, WANA JAMBO LAO

HASHEEM Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanaoibeza timu hiyo watakutana na balaa kwenye ligi na mashindano mengine. Msimu wa 2022/23 Azam FC iligotea nafasi ya tatu kwenye ligi na lishuhudia Yanga ikitwaa taji la ligi. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo iligotea nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Ngao ya…

Read More

JEMBE JIPYA LAANZA KAZI MSIMBAZI

WAKIWA kwenye milima ya Uluguru, Morogoro wachezaji wa Simba wameungana na kipa mpya Ayoub Lakred. Kipa huyo ni ingizo jipya ndani ya Simba ambapo anakuwa ni kipa wa kimataifa yeye ni raia wa Morocco na watani zao wa jadi Yanga wana kipa raia wa Mali, mdaka mishale Djigui Diarra. Agosti 15 ilikuwa ni siku yake…

Read More

YANGA YAIPIGIA HESABU ASAS DJIBOUT

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanatarajia kuanza mazoezi katika kambi iliyopo AVIC Town, Kugamboni. Timu ya Yanga imetoka kucheza mashindano ya Ngao ya Jamii ilipoteza kwa penalti mchezo wa fainali dhidi ya Simba. Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema, “Wachezaji wote wapo vizuri na wanatarajia kuanza…

Read More

IHEFU YAANZA KWA KUPOTEZA LIGI KUU BARA, GEITA KICHEKO

GEITA Gold inaandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kukomba pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24. Ni Agosti 15 rasmi ligi  imeanza ambapo Geita Gold walikuwa ugenini walipokaribishwa na Ihefu. Ikumukwe kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga ambao walitwaa taji hilo wakiwa na jumla ya pointi 78. Yanga walikuwa…

Read More

KINAWAKA LEO LIGI KUU BARA

HATIMAYE kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuanza leo Agosti 2023 kwa baadhi ya mechi kupigwa viwanjani. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 ambapo mabingwa walikuwa ni Yanga tarehe kama ya leo Agosti 15 ligi ilianza na mchezo wa ufunguzi ilikuwa Ihefu 0-1 Ruvu Shooting. Ihefu timu ya kwanza kuitungua Yanga kwenye ligi inakwenda kufungua…

Read More

UCHAWI WA ALLY SALIM NA PENALTI UPO HAPA

MLINDA mlango wa Simba, Ally Salim, amefunguka kuwa siri kubwa ya kuokoa penalti tatu kati ya nne zilizopigwa na Yanga katika mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii, ni maelekezo aliyopewa na kocha wao wa makipa, Daniel Cadena. Salim jana Jumapili alifanikiwa kuibuka shujaa kwa kuokoa penalti tatu za Yanga zilizopigwa na Pacome Zouzoua, Yao…

Read More

KULINDANA NI MUHIMU, HAKI PIA IZINGATIWE

KILA mmoja anatambua kwamba pazia la Ligi Kuu Bara linakwenda kufunguliwa leo ambapo kuna mechi zitakazoanza kuchezwa katika viwanja tofauti. Yanga ambao ni mabingwa watetezi hawa kete yao ya kwanza itakuwa dhidi ya KMC wote ni watoto wa mjini. Simba iliyogotea nafasi ya pili kibarua chake ni dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa ugenini kwenye mchezo…

Read More

SIMBA WAMESHINDA DHIDI YA TIMU ILIYOONYESHA UBORA

USHINDI wa Ngao ya Jamii ambao wameupata Simba dhidi ya Yanga ni bahati ya mtende kutokana na kiwango cha chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa Simba. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulikuwa unasoma Yanga 0-0 Simba na kupelekea mshindi apatikane kwa penalti. Katika Ngao ya Jamii kwenye mchezo wa fainali Agosti…

Read More

SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII, SALIM SHUJAA

NGAO ya Jamii ni mali ya Simba baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ndani ya Uwanja wa Mkwakwani. Ilikuwa ni fainali ambayo Yanga walikuwa na nafasi kubwa kwenye upande wa kupata matokeo ndani ya dakika 90 kutokana na mashambulizi waliyokuwa wakiyapeleka kwa Ally Salim. Hilo pia limedhihirishwa na nahodha wa Yanga Bakari…

Read More