Betway yatoa elimu ya kubashiri kwa uwajibikaji Barani Afrika

Betway imetoa wito kwa wachezaji wote kutafakari juu ya tabia zao za kubashiri na kukumbatia mtazamo mzuri wenye uwiano bora zaidi katika uchezaji.

Betway imetoa wito huo katika mwezi wote wa Novemba ambapo imekuwa ikitoa elimu kuhusu kubashiri kwa uwajibikaji kupitia kampeni yenye kauli mbiu “Kubashiri kwa Uwajibikaji”.

“Betway inathibitisha tena dhamira yake ya kuhimiza uchezaji salama, wenye ufahamu na uwajibikaji barani Afrika,” alisema Calvin Mhina, ambaye ni Meneja Masoko wa Betway.

Alifafanua kwamba katika maeneo ambapo michezo ya kubashiri inaendelea kukua kwa kasi, Betway inaongoza jitihada za kuhakikisha kwamba burudani haiwi kwa gharama ya ustawi wa watu.

“Katika mwezi huu wa Novemba chapa hii inasisitiza ujumbe mkuu wa mambo manne yanayounda kiini cha uchezaji wa kubashiri kwa uwajibikaji,” alieleza.

Kwa mujibu wa Mhina, mambo hayo manne ni pamoja na kutokufukuzia hasara zako kwani kubashiri kunapaswa kuwa kwa ajili ya burudani na sio njia ya kurudisha pesa ulizopoteza. Kujaribu kurudisha hasara mara nyingi husababisha msongo wa kifedha na kihisia.

Betway pia imewakumbusha wachezaji kukumbuka kupumzika ili pamoja na mambo mengine mhusika aweze kujipanga upya, arudi akiwa na akili tulivu na kuongeza kuwa kupumzika kunasaidia kudhibiti hali na maamuzi.

“Ni muhimu pia kuwa na mpango, yaani kuweka mipaka ya muda na kiasi cha fedha kabla ya kucheza. “Jua wakati wa kuacga na ushikamane na mpango wako,” aliongeza meneja huyo.

Aliwakumbusha wanaobashiri kukumbuka kudhibiti uchezaji wao kwani kubashiri ni burudani na sio suluhu la changamoto za maisha.

Meneja huyo alifafanua kuwa kubashiri kwa uwajibikaji sio ujumbe tu bali ni harakati. “Tunaamini kwa kuwawezesha wachezaji wetu kupitia zana na maarifa sahihi , tunawza kujenga mazingira salama na endelevu zaidiya kubashiri kwa wote.

Alibainisha kuwa katika mwezi huu wa Novemba Betway imezindua mfulululizo wa program za elimu, kampeni za mitandao ya kijamii na shughuli za kijamii katika masoko yake mbalimbali barani Afrika.

Juhudi hizi, alisema Mhina, zimekusudia kuongeza uelewa, kutoka rasilimali za msaada na kuhamasisha mijadala ya wazi juhusu tabia za kutabiri.

“Kama sehemu ya kujitolea kwa muda mrefu, Betway pia inatoa zana mbalimbali za kubashiri kwa uwajibikaji kwenye tovuti yake , ikiwemo mipaka ya fedha, chaguo la kujizuia mwenyewe kwa muda na huduma za msaada wa kitaalamu,” alisema Mhina.

Ameeleza pia kwamba katika mwezi wa Novemba, Betway imewaalika wachezaji wote kusimama kidogo, kutafakari na kubashiri kwa njia ya uwajibikaji.