Dube, Zouzoua na Ecua Waongoza Mashambulizi ya Yanga Dhidi ya Waarabu wa Morocco

VIKOSI vinavyoanza kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya wenyeji, Young Africans Sc dhidi ya vigogo wa Morocco, AS Far Rabat.

Mechi hiyo ya Kundi B la CAFCL utapigwa katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni hii.

Kocha wa Yanga SC, Pedro Gonçalves amemrejesha Mudathir Yahya kwenye kikosi kinachoanza huku Mohammed Doumbia akianzia benchi.

Golini anaanza Djigui Diara, mabeki Israh Mwenda, Mohamed Husein, Ibrahim Bacca na Dickson Job wakati Duke Abuya akiendelea kuaminiwa kwenye safu ya kiungo sambamba na Maxi Nzengeli na Mudathir Yahaya

Prince Mpumelelo Dube anaongoza safu ya ushambuliaji akisaidiwa na Pacome Zouzoua na Celestin Ecua