Ahmed Ally: Ukiona kuna timu inaongoza ligi imetuzidi mchezo

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa ikiwa kutakuwa na timu inaongoza ligi basi itakuwa imewazidi mchezo.

Msimu wa 2025/26 vinara wa ligi ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves ni mechi nne wamecheza wakiwa na pointi 10 kibindoni.

Simba SC kwenye msimamo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270,wamekusanya pointi 9 kibindoni.

Mchezo wa tatu kabla ya ligi kusimama ilikuwa ugenini ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania, wafungaji walikuwa ni Edward Songo kwa JKT Tanzania yale ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu na Jonathan Sowah.

Ahmed amesema: “Kwenye msimu huu tumefanya kazi kubwa katika mechi zetu kutafuta matokeo. Ukiona kuna timu inaongoza ligi kwa sasa basi inabidi utambue kwamba imetuzidi mechi hivyo tu kwenye matokeo tumekuwa imara,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.