JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League

JKT Tanzania 1-2 Simba SC ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuyo Novemba 8,2025.

Katika mchezo huo wenyeji JKT Tanzania walitangulia kupata bao la kuongoza kipindi cha pili kwa kuwa dakika 45 za mwanzo hakuna timu ambayo iliona lango la mpinzani.

Ni Edward Songo dakika ya 60 alifunga bao la kuongoza akimtungua Yakoub Suleman ambaye alianza langoni kwenye mchezo huo mbele ya waajiri wake wa zamani.

Iliwachukua Simba SC dakika 4 kuweka usawa kupitia kwa Wilson Nangu ambaye ni beki wa zamani waJKT Tanzania alipachika bao hilo dakika ya 64.

Jonathan Sowah ambaye naye alianzia benchi kwenye mchezo huo alipachika bao la ushindi dakika ya 76 likipeleka pointi tatu unyamani.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kuongoza ligi wakifikisha jumla ya pointi 9 baada ya mechi tatu msimu wa 2025/26.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.