Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara Novemba 8,2025

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa leo Novemba 8,2025 Jumamosi ya kazikazi kwa wababe kushuka uwanjani kusaka ushindi.

Kutakuwa na mechi kubwa mbili katika viwanja tofauti ni Dar na Mwanza ambao watakuwa wanashuhudia mechi za ushindani.

Saa 10:00 jioni Pamba Jiji vs Singida Black Stars, itachezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwenye msimamo wa ligi, Pamba Jiji FC nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 8 baada ya kucheza mechi 5 inakutana na Singida Black Stars ambayo ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 6 baada ya mechi 2.

 Saa 1:00 usiku, JKT Tanzania VS Simba SC, Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

JKT Tanzania kwenye msimamo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 7 baada ya mechi 5 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya 7 na pointi 6 baada ya mechi 2.

Zote zitakuwa mubashara kupitia AzamSports1HD.

 

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.