Meneja Mkuu Dimitar Pentev amewasili Tanzania akitokea Botswana kwa ajili ya kuanza kazi kukifundisha kikosi cha Simba SC.
Pentev ameongozana na msaidizi wake, Boyko Kamenov ambaye watafanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa na Seleman Matola katika benchi la ufundi.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa meneja huyo ataanza majukumu yake mara moja na Jumapili ataonana na wachezaji pamoja na viongozi.
“Tayari ameshaanza kazi kwa lugha rahisi hasa ukizingatia ameshawasili Tanzania. Anakuwa meneja mkuu kwa kuwa ameongezewa majukumu mengi zaidi hivyo hili linaweza kuonekana ni jambo la ajabu kwa dunia ya tatu lakini kule mbele ipo hivyo.
“Ipo kawaida na maendeleo ya soka yanatambua uwepo wa meneja mkuu. Tunaamini kwamba atafanya kazi kubwa kwa ushirikiano na wengine, viongozi kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa. Huyu ni bora na kila mmoja anakuwa bora kwa wakati wake,” .
Huyu ni mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ambaye alikuwa na kikosi mwanzo wa msimu na sasa ameajiriwa Raja Casablanca.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.