KAIMA Kocha Mkuu wa Simba, Hemed Suleiman Morocco hatokuwa tena sehemu ya benchi la ufundi katika michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba SC baada ya kutinga hatua ya pili kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana itakabiliwa na Nsingizini Hotspurs ya nchini Eswatini.
Mchezo wa kwanza Simba SC itakuwa ugenini unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 17-19 baada ya mchezo huo Simba SC itarejea Dar, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 24-25, mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi kusaka tiketi ya kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwenye mechi hizo zijazo kimataifa Simba SC haitakuwa na Morocco kwenye benchi la ufundi kwa kuwa makubaliano ilikuwa ni katika mchezo mmoja pekee wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana.
Kikosi cha Simba kitaendelea kuwa chini ya kocha msaidizi Suleiman Matola ambaye hakuwa katika benchi katika mchezo uliopita Septemba 28 2025 kutokakana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Simba SC kupitia ukurasa wa Instagram wametuma shukrani zao kwa kuandika namna hii: “Shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuongoza kikosi chetu katika mchezo muhimu wa jana wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, na kufanikiwa kutuvusha.
“Shukrani pia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco ambaye ni Kocha wa Taifa Stars kujiunga nasi,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.