Oscar Mirambo Ateuliwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo kuanzia Oktoba 1, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, uteuzi huo unakuja kufuatia kumalizika kwa mkataba wa aliyekuwa Katibu Mkuu, Kidao Wilfred, ambao unahitimishwa tarehe 30 Septemba 2025.

Mirambo, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, ataingia rasmi kwenye majukumu yake mapya mara tu mkataba wa Kidao utakapomalizika. Atasimamia shughuli zote za kila siku za Sekretarieti ya TFF hadi pale Kamati ya Utendaji ya TFF itakapotoa uamuzi mwingine kuhusu nafasi hiyo.