UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa una kikosi imara na chenye uwezo wa kuleta ushindani kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika.
Septemba 10 2025 ilikuwa ni kilele cha tamasha la Simba Day, Uwanja wa Mkapa na ilikuwa ni Full House baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja na kushangilia mwanzo mwisho.
Katika tamasha hilo ambalo ni msimu wake wa 17 kulikuwa na burudani nyingi huku msanii wa muziki wa kizazi kipya Mbosso akifanya Perfomance katika kiwango kikubwa na King Kiba alikuwepo pia.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa kila Mwanasimba amekiona kikosi na anatambua uimara ulipo na ubora licha ya kuwa ni mchezo mmoja wa ushindani.
“Ulikuwa ni mchezo wa kirafiki mzuri licha ya kwamba ni mchezo mmoja bado Wanasimba wamepata nafasi ya kuona uimara wa kikosi. Kila mchezaji alipata nafasi yakucheza kulingana na mpango kazi wa benchi la ufundi.
“Kuna kazi kubwa inakuja na tunaamini kwamba furaha ipo kwa msimu mpya, kila kitu ni maandalizi na sisi tunafanya maandalizi kwa umakini.”.
Mchezo ujao kwa Simba SC ni Septemba 16 2025 ambao utakuwa ni wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkapa dhidi ya mtani wake wa jadi Yanga SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.