TANZANIA YAVUNA POINTI MOJA MBELE YA CONGO

HEMED Suleiman, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameweka wazi kuwa hawakucheza vizuri kama ambavyo walitarajia katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya timu ya taifa ya Congo Brazzaville .

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Alphonce Masamba Debat ulisoma Congo Brazzaville 1-1 Tanzania. Ni Dechan Moussavou Lingard alifungua pazia la kufunga dakika ya 69. Shuti lake akiwa nje ya 18 lilimshinda mlinda mlango Yacoub Suleiman ambaye alianza kikosi cha kwanza.

Bao la kuweka usawa lilifungwa na Seleman Mwalimu Ali dakika ya 84. Mwalimu katika mchezo huo alianzia benchi.Kituo kinachofuata kwa Tanzania ni Septemba 9 2025 dhidi ya Niger, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Kocha Seleman ameweka amebainisha kuwa walikutana na ushindani mkubwa kwenye mchezo huo hivyo makosa ambayo yametokea watafanyia kazi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mchezo ujao.

“Tunamshukuru Mungu mchezo umamelizika salama, hatukucheza vizuri kama ambavyo tulitarajia na mwisho tumepata pointi moja hivyo tutafanyia kazi makosa ili kuwa imara wakati ujao,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.