Clatous Chama msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya uzi wa Singida Black Stars kwa changamoto mpya baada ya mkataba wake kuisha ndani ya Yanga SC.
Tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake huku akiwa amekabidhiwa jezi namba 7 kwa ajili ya mazoezi ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.
Chama Septemba 4 2025 alianza kazi ndani ya kikosi cha Singida Black Stars ikiwa ni ingizo jipya kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Gamondi alifanya kazi na Chama akiwa na uzi wa Yanga SC kabla ya kuondoka wanakutana naye kwa mara nyingine tena.
Kikosi cha Singida Black Stars kinashiriki mashindano ya Kagame Cup yanayofanyika katika ardhi ya Tanzania, leo Septemba 5 2025 Chama ameanza benchi kwenye kikosi ambacho kinacheza na Polisi ya Kenya.
Huenda akapewa jezi namba 17 ambayo ni chaguo lake la kwanza alikuwa akivaa hiyo hata alipokuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Anaungana na Khalid Aucho ambaye naye yupo ndani ya Singida Black Stars ila kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Uganda.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.