AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amewaomba mashabiki wa Simba SC kufanya kila linalowezakena lakini wasikosekana Septemba 10 2025 Uwanja wa Mkapa kwenye tamasha la Simba Day.
Katika tukio hilo kubwa msimu wa 17 wachezaji, benchi la ufundi watatambulishwa wakiwa kwenye jezi mpya za msimu wa 2025/26 na wanatarajia kucheza mchezo wa karafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Ahmed amesema: “Nichukue nafasi hii kuwaalika kwenye Simba Day ambayo itafanyika Septemba 10, 2025. Ukubwa wa tamasha letu, ubora wa tamasha letu umetokana na Wanasimba kujitokeza kwa wingi. Kama mngekuwa hamjitokezi lingekuwa tamasha dogo kama matamasha mengine nchini na Afrika.
“Tulishafanya vizuri huko nyuma kwa kujaza uwanja na sasa shughuli muhimu ya kufanya. Kwahiyo ndugu zangu kama hujawahi kwenda Simba Day ifanye hii kuwa Simba Day yako ya kwanza kuja uwanjani.
“Mwanakunduchi usikubali kubaki nyumbani siku hiyo, usikubali kubaki kazini siku hiyo. Hii ni siku ambayo kila Mwanasimba anapaswa kujivunia, watu wengine wanatamani kuwa na siku kama hii. Sisi Wanasimba hatupaswi kuichukulia kawaida siku hiyo, hatupaswi kuichukulia siku isiyo na thamani.
“Hii ni Simba Day tiketi zinawahi kuisha, kama tawi mngewahi kununua mapema ili kuwa na uhakika wa kuwepo uwanjani siku hiyo. Nitoe pongezi kwa uzinduzi mkubwa ambao mmeufanya.”
Shughuli mbalimbali za kijamii zimeendelea ikiwa ni ufunguaji wa matawi miongoni mwa hayo ni Tawi la Wekundu Kunduchi Mtongani na Septemba 5 2025 tawi la Simba SC VIP A Magomeni limezinduliwa.
Tukio jingine ambalo limefanywa na Simba SC, Septemba 5 2025 ni kula chakula cha pamoja na watoto wenye uhitaji katika kituo cha watoto yatima cha Umra kilichopo Magomeni, Mikumi Dar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.