INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz anatajwa kuwa na balaa zito kwenye uwanja wa mazoezi.
Ni kiungo ambaye anatajwa kuwa mbeba mikoba ya nyota Aziz Ki ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya.
Anaitwa Mohammed Doumbia inaelezwa kuwa katika kambi ya timu hiyo iliyopo Kijiji cha Avic Town, Kigamboni anafanya kazi kubwa katika uwanja wa mazoezi ikiwa ni balaa zito.
Doumbia ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga SC msimu ujao, amekuja kuwa mrithi wa Stephen Aziz Ki aliyeuzwa msimu uliopita kuelekea Wydad Casablanca ya Morocco.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa wachezaji wote kambini wanafanya kazi kubwa kuelekea msimu mpya hivyo wanaamini kazi itakuwa kubwa ndani ya uwanja.
“Wachezaji wote waliopo katika kikosi cha Yanga SC wanafanya kazi kubwa kwenye kutimiza majukumu hilo lipo wazi. Sio Doumbia na wengine kazi yao ni kubwa chini ya benchi la ufundi na tunaamini tutakuwa na mwendo mzuri msimu mpya,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.