WAARABU Wadi Degla SC 0-2 Simba SC ni matokeo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Agost 26 2025 ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2025/26. Simba SC imeweka kambi Misri na inatarajiwa kurejea Tanzania Agosti 28 2025.
Simba SC imecheza jumla ya mechi nne, ikipata ushindi kwenye mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Nyota Elie Mpanzu aliipa Simba goli la uongozi dakika ya 73 akiwa nje ya 18 mbele ya duara la katikati mwa uwanja. Mpanzu alifunga goli hilo kwa shuti kali ambalo lilizama mazima nyavuni.
Wadi Degla walishuhudia dakika 79 nyavu zikitikisika kupitia kwa Kibu Denis ambaye alifunga kwa kutumia pasi ya kiungo mshambuliaji Jean Ahoua.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza ilikuwa namna hii:-
Moussa Camara, Ladack Chasambi, Naby Camara, Rushine De Reuck, Chamou Karaboue, Morrice Abraham, Kibu Denis, Jean Ahoua, Neo Maema, Elie Mpanzu na Steven Mukwala.
Wachezaji wa Akiba:
Hussein Abel, Alexander Erasto, David Kameta, Anthony Mligo, Saleh Karabaka, Alassane Kante, Mohammed Bajaber, Jonathan Sowah, Bashiru Salum, Joshua Mutale, Awesu Ally, Mzamiru Yassin, Valentino Mashaka, Semfuko Charles, Hussein Mbegu.