MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC raia wa Ghana, Jonathan Sowah anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC utakaopigwa Septemba 16 2025, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa Ngao ya Jamii ni maalumu kwa ajili ya kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Mshambuliaji huyo mpya Sowah hatocheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye fainali dhidi ya Yanga SC.
Sowah alipata kadi hiyo nyekundu katika mchezo wa Fainali ya Kombe la CRDB ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar akiwa anaichezea Singida Black Stars kabla ya kutambulishwa Simba SC kuwa ingizo jipya na yupo na timu kambini Misri.
Taarifa zinaeleza kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC, Neo Maema ambaye alitambulishwa Simba SC Agosti 21 2025 akitokea Mamelod Sundowns huenda akabeba mikoba yake kwenye mchezo huo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.