RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo.
Karia ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ya Shirikisho la soka Afrika CAF, alichaguliwa tena kama Rais wa TFF katika Uchaguzi wa kupata Kamati mpya ya Utendaji ya TFF uliofanyika Jijini Tanga mnamo Agosti 16, 2025 akiwa mgombea pekee.
“Kuchaguliwa kwako tena ni ishara ya imani ya Wanachama wako kwa uongozi wako bora, najivunia sana bidii yako na kujitolea kwa maendeleo na ukuaji wa soka Tanzania,”—alisema Dkt. Motsepe
Vilevile Motsepe ameipongeza Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa, na amesema CAF itaendelea kusaidia kukuza mpira wa miguu Tanzania na Kanda ya CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati).