CAF YATOZA KENYA FAINI YA MILIONI 127, YAONYA KUHAMISHIA MECHI NJE

Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) imeipiga Kenya faini ya dola 50,000 za Marekani (sawa na takribani TZS milioni 127.8) kutokana na makosa ya kiusalama yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Morocco uliofanyika kwenye Uwanja wa Moi, Kasarani.

CAF imeonya kuwa iwapo kasoro hizo zitaendelea, mechi zijazo za timu ya taifa ya Kenya zinaweza kuhamishiwa nchini Uganda au Tanzania.