AZAM YAMSAJILI EDWARD MANYAMA KWA MKATABA WA MWAKA MMOJA

Klabu ya Azam FC imethibitisha kumsajili beki wa kati Edward Charles Manyama kwa mkataba wa mwaka mmoja, utakaomuweka ndani ya kikosi hicho hadi mwaka 2026.

Manyama (31), raia wa Tanzania, ana historia ya kuchezea vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu Tanzania Bara, vikiwemo Namungo FC, Azam FC, Ruvu Shooting na Singida Black Stars. Anarejea kwa Wanalambalamba baada ya kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars.

Ujio wa Manyama unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Azam FC kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu, huku benchi la ufundi likiendelea kufanya maboresho ya kikosi chao.