DILI la MZIZE LIPO HIVI: SALEH JEMBE AFICHUA TATIZO LILIPO – AWAAMBIA YANGA – ”ANATAFUTA MAISHA”..

Mchambuzi mahiri wa soka nchini, Saleh Jembe, amesema kuwa ubora wa klabu kongwe za Simba SC na Yanga SC umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa kiwango cha Timu ya Taifa, Taifa Stars.

Akizungumza kuhusu mashindano ya CHAN, Jembe alisema Stars imeanza vizuri na anaamini itaendelea na mwenendo huo hadi mwisho.

“Ubora wa wachezaji wanaocheza Simba na Yanga umekuwa msaada mkubwa kwa Taifa Stars. Imeanza vizuri CHAN, naamini itamaliza vizuri,” alisema Jembe.

Stars kwa sasa iko katika hatua za awali za mashindano hayo, ikionyesha mchezo mzuri na mshikamano wa kikosi.