KOCHA Fadlu Davids alipomuona kijana kwenye majukumu yake inaelezwa kuwa akawaambia mabosi wa Simba SC anahitaji saini ya Antony Mligo aliyekuwa ndani ya Namungo FC.
Haya ni maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo Simba SC ilipishana na ubingwa msimu wa 2024/25 ulikwenda kwa watani zao wa jadi Yanga SC.
Rasmi Agosti 5 2025 beki huyo ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC ambacho kimeweka kambi nchini Misri.
Agosti 4 2025 aliwaaga Namungo FC hivyo atakuwa katika changamoto mpya 2025/26. Hivyo atakuwa kwenye uzi mpya kupambania majukumu yake katika kusaka ushindi ndani ya Simba SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.