CAF YAMFUTA KAZI MKURUGENZI MKUU WA WAAMUZI KUFUATIA SAKATA LA FAINALI YA WAFCON YA WANAWAKE

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limemfuta kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Waamuzi, Désiré Noumandiez Doué, kwa makosa yaliyofanywa katika Kombe la Afrika la Wanawake.

Haya yanajiri baada ya Shirikisho la soka la Morocco (FRMF), kuwashutumu Waamuzi akiwemo Mukansanga Salima na Umutesi Alice kwa kuchezesha isivyo Fainali ya Kombe la Afrika kwa Wanawake.
Mukansanga Salima aliongoza timu ya waamuzi waliokuwa wakifuatilia picha za VAR Nigeria iliposhinda 3-2 dhidi ya Morocco kwenye fainali.

Athari kwa Waamuzi imeanza kuonekana kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Morocco, raia wa Ivory Coast Désiré Noumandiez Doué, ambaye alikuwa mwakilishi wa Waamuzi katika CAF akifukuzwa kazi.
CAF pia inatajwa kuchunguza masuala ya taaluma mbovu kwa Waamuzi wa soka barani Afrika, jambo ambalo linaweza kuwafanya baadhi ya Waamuzi wa Kimataifa kupokonywa haki yao ya kuwa Waamuzi wa mechi kubwa.