YANGA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wa kazi Duke Abuya raia wa Kenya.
Abuya ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika kikosi cha Yanga SC kilichotwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2024/25 kikiwa na pointi 82 kibindoni baada ya mechi 30.
Ni mechi 27 alicheza akikomba dakika 1,496 alihusika kwenye mabao matano kati ya 83 yaliyofungwa na timu hiyo, alifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao yupo mpaka 2027.
Julai 27 2025 Yanga SC iliwatambulisha wachezaji wawili, ilianza na kumtambulisha Aboubakar Nizar maarufu kama Ninju na ikamaliza na utambulisho wa Duke ambaye ameogeza mkataba wa miaka miwili ndani ya Jangwani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.